Villagers of South Unguja Pete acquiring knowledge about the fight against AIDS through Jihadhari magazine released by Zanzibar AIDS Commission
Children at ZAPHA+
ZAC Monitoring and Evaluation Coordinator Mr. Ali Kimwaga in one of the M&E meeting
Theatre for Social Development (THESODE) on the stage
Group Picture during World AIDS day climax 2015
Participants attended National Youth Forum in Zanzibar
Group Picture during World AIDS day climax, 1 December 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Watendaji wa Wizara yake ikiwemo Tume ya UKIMWI ambayo imehamishiwa Wizara hiyo.

ZAC Chairperson

Welcome to the Zanzibar AIDS Commission (ZAC) Website. We hope that the ZAC website will serve to give a closer picture about ZAC...Read More

RISALA YA KAIMU MWENYEKITI WA BODI YA TUME YA UKIMWI ZANZIBAR BI. HASINA HAMADI KATIKA SIKU YA MAADHIMISHO YA UKIMWI DUNIANI- DISEMBA 01, 2016

MHESHIMIWA MGENI RASMI, WAZIRI WA NCHI OMPR

MHESHIMIWA MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

WAHESHIMIWA MAWAZIRI

WAHESHIMIWA WAKUU WA WILAYA

WAHESHIMIWA MAKAMISHNA WA TUME YA UKIMWI

WAHESHIMIWA MAKATIBU WAKUU 

NDUGU WASHIRIKA WA MAENDELEO

NDUGU MKURUGENZI MTENDAJI WA TUME YA UKIMWI 

WAGENI WAALIKWA, MABIBI NA MABWANA

ASSALAAMU ALAYKUM,

Assallam Alleykum, 

Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema ndiye wa kushukuriwa na naomba nichukue nafasi hii kwa niaba yenu kumshukuru kwa kutujaalia uhai na uzima siku hii adhimu ya leo. Aidha nichukue nafasi hii kumshukuru tena Subha’nahuu Wataala kwa kutuwezesha kukutana tena ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.

Ndugu Wananchi,

Kwa mnasaba wa hafla yetu hii,  leo tunaungana na Jamii ya Kimataifa na mataifa mengine Duniani katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI Duniani (International World AIDS Day) ambayo  huadhimishwa kila ifikapo tarehe 01 Disemba Duniani kote na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI yaani UNAIDS.  Siku ya Maadhimisho ya UKIMWI Duniani pamoja na mambo mengine huwa ni ukumbusho kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na Jamii ya Kimataifa kwa ujumla juu ya azimio lenye lengo la kuwa na jamii iliyo huru  na maambukizi ya UKIMWI.

Harakati za maadhimisho ya siku hii kama wengi wetu tunavyofahamu hulenga zaidi katika kuongeza uelewa na kuishajihisha jamii kufahamu mafanikio na changamoto zinazoikabili dunia juu ya tatizo la maambukizi ya UKIMWI na kuandaa mikakati mbali mbali katika kukabiliana nalo.

Ndugu Wananchi,

Maadhimisho hayo kama tunavyoelewa  hubebwa na kauli mbiu na kwa Mwaka Huu inasema “PATA HAKI STAHIKI ZA HUDUMA ZA UKIMWI’’, kauli   ambayo inasisitiza   umuhimu wa watu kuzitumia huduma muafaka zinazohusiana na kinga au tiba dhidi ya maradhi ya UKIMWI. Kuwepo kwa  huduma  hizi ni  muhimu sana katika kupunguza kasi ya maambukizi mapya  ya  Virusi Vinavyosababisha UKIMWI (VVU) 

Ndugu Wananchi,

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Tume ya UKIMWI Zanzibar imeweza kufanikisha mambo mbali katika kukabiliana na janga la UKIMWI hapa visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na wadau mbamabali wakiwemo washirika wetu wa maendeleo.

Katika risala yangu ya siku kama ya leo mwaka jana niliainisha  mipango ya muda mfupi na kazi iliyopangwa na kutekelezwa katika kupambana na janga hili ikiwemo tathmini iliyoangalia shughuli zilizofanyika maeneo yote manne makuu ya mwitiko wa UKIMWI yakiwemo: kinga, tiba, matunzo na kupunguza athari ya UKIMWI, uwekaji wa mazingira wezeshi, ufuatiliaji na tathmini. Tume ya UKIMWI  Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wake imeendelea kutekeleza shughuli zake mbali mbali na kuweza kufanikisha yafuatayo:-

a) Kuandaa Mpango Mkakati wa tatu wa Kitaifa wa mapambano dhidi ya UKIMWI 

b) Kuandaa mipango kazi ya utekelezaji ya kukabiliana na tabia na maeneo hatarishi kwa kushirikiana na Wilaya husika Unguja na Pemba kwa lengo la kupunguza kiwango cha maambukizi mapya ya UKIMWI.

c) Kuanda programu maalum  kwa vijana zinazolenga katika kuibua changamoto zinazowakabili  zenye lengo la kuwaepusha na maambukizi ya UKIMWI na unyanyasaji wa kijinsia ziliweza kuibuliwa kupitia mikutano mbali mbali ya Vijana Unguja na Pemba.

d) Kufanya utafiti juu ya uelewa, mtazamo na matendo ya tabia hatarishi kwa vijana zinazopelekea maambukizi ya UKIMWI.

e) Kuandaa mkutano wa Kitaifa wa Vijana uliowashirikisha vijana kutoka asasi za kiraia, na  sekta mbali mbali  za serikali kwa lengo la kujadiliana juu ya taarifa zinazoashiria kuengezeka kwa tabia hatarishi kwa vijana. 

f) Kuandaa kampeni maalum iitwayo “Kijana Kataa UKIMWI” yenye lengo la kuwatanabahisha vijana juu ya tabia hatarishi zinazopelekea kupata maambukizi ya VVU

g) Hadi kufikia September, Jumla ya mama wajawazito 29,490 walipata huduma ya kupima VVU na kati yao 138 (0.5%) waligundulika na VVU 

h) Hadi kufikia Septemberer, Jumla ya watoto 171 waliozaliwa na mama wajawazito walichunguzwa maambukizi ya VVU. Kati yao 4 tu ndio waligundulika na VVU ambapo ni sawa na asilimia 0.02  

i) Hadi kufikia September, Jumla ya wagonjwa wapya 525 waliorodheshwa kwenye klniki za matibabu na kati ya hao wagonjwa 483 (92%) walianzishiwa dawa za ARVs  

Aidha  nichukue nafasi hii pia kuwajuilisha kwamba Tume ya UKIMWI  na Afisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibari kwa kushirikiana na Kamisheni ya UKIMWI na Afisi ya Mtakwimu Mkuu Tanzania Bara zinaendelea na Utafiti wa kuangalia viashiria vya maambukizi ya UKIMWI ikiwemo kiwango cha watu wanaoishi na VV na idaddi ya maambukizi mapya katika mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Hivyo nichukuwe nafasi hii kuwaomba wananchi wote ambao watakaofikiwa na utafiti huu kukubali kushiriki kikamilifu ili kuweza kufanikisha malengo ya utafiti huu muhimu kwa Taifa letu. Kwani matokeo ya utafiti huu yanaumuhimu mkubwa katika kupanga na kutowa huduma zinazohusiana na maradhi ya UKIMWI. 

Ndugu Wananchi,

Napenda kuchukua nafasi hii kutoa indhari kwamba tuendeleee kuchukua hadhari juu ya suala zima la maambukizi ya UKIMWI, juhudi na mafanikio  yaliyokwisha patikana ziwe chachu ya kusonga mbele zaidi, yafaa tuelewe kwamba janga la UKIMWI bado ni tishio duniani kote ikiwemo visiwa vyetu vya Zanzibar. Inatupasa kuchukua juhudi za makusudi kwa kila mmoja wetu katika dhamira ya kweli na mashirikiano ya kila mmoja wetu ikiwemo watu binafsi, familia, Shehia, wilaya na Taifa kwa ujumla, kwa kufanya hivyo tutakuwa na  msingi imara utakaotufikisha katika matarajio ya kuijenga Zanzibar bila ya UKIMWI. 

Ndugu Wananchi,

Mwisho basi nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao kwa njia moja au nyengine wamekuwa wakitoa mchango wao katika Mapambano Dhidi ya UKIMWI hapa Zanzibar. Tume ya UKIMWI na Serikali kwa ujumla  inathamini sana juhudi zao na tunawaomba waendelee katika kutuunga mkono ili tuweze kupata ushindi na mafanikio zaidi na InshaAllah Mwenyezi Mungu atatusaidia. 

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

 

 

CDC.jpgCHAI.jpgGlobal Fund Logo.pngLOGO ONE UN.jpgPEPFAR.pngUNAIDS.jpgUNDP.jpgUNFPA.jpgUNICEF.pngUSAID.jpgWHO.pngWORLDBANK_LOGO.jpg