Villagers of South Unguja Pete acquiring knowledge about the fight against AIDS through Jihadhari magazine released by Zanzibar AIDS Commission
Children at ZAPHA+
ZAC Monitoring and Evaluation Coordinator Mr. Ali Kimwaga in one of the M&E meeting
Theatre for Social Development (THESODE) on the stage
Group Picture during World AIDS day climax 2015
Participants attended National Youth Forum in Zanzibar
Group Picture during World AIDS day climax, 1 December 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Watendaji wa Wizara yake ikiwemo Tume ya UKIMWI ambayo imehamishiwa Wizara hiyo.

ZAC Chairperson

Welcome to the Zanzibar AIDS Commission (ZAC) Website. We hope that the ZAC website will serve to give a closer picture about ZAC...Read More

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza alisema jitihada na umoja miongoni mwa Watendaji wa Taasisi za Serikali ndio njia pekee itakayoleta ufanisi na faraja kwa wananchi wanaowahudumia.

Nd. Meza alisema hayo kwa mara ya kwanza tokea alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Zanzibar kushika wadhifa huo wakati akizungumza na Viongozi na maafisa wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema kazi kwa watumishi wa Umma ni kama Kijiji na majirani wanaopaswa kuwajibika kwa kuzingatia ushirikiano lengo likiwa ni kutekeleza sheria na miongozo ya Serikali iliyowekwa katika kuwatumikia Wananchi wote.

Nd. Joseph Meza aliwakumbusha wafanyakazi kuwajibika katika kufuata muelekea wa mfumo wa Serikali kwa kuangalia jukumu linalohitaji kutekelezwa mwanzo kwa mujibu wa uwezo uliopo katika Taasisi husika.

Alieleza kwamba uwajibikaji makazini ni vyema ukaenda kwa haraka zaidi ili kufidia muda wa utekelezaji wa Serikali iliyopo madarakani ambao ulipungua kutokana na kurudiwa kwa uchaguzi Mkuu uliopita wa Zanzibar.

Mapema akimkaribi Nd. Joseph Abdulla Meza kuanza kazi rasmi katika Ofisi yake mpya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji alisema watendaji wa Wizara hiyo wanapaswa kutumia muda wa ziada katika kuhakikisha Bajeti ya Wizara hiyo inakamilika katika muda iliyopangiwa.

Nd. Ahmad alisema zipo changamoto zitazohitajika kuchukuliwa hatua za haraka katika kukamilisha kazi hiyo inafanikiwa licha ya mabadiliko ya uhamisho kwa baadhi ya Taasisi kuingia katika Wizara hiyo.

Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kutokana na mabadiliko ya Mawizara yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar imepokea baadhi ya Taasisi kutoka Wizara zilizovunjwa.

Taasisi hizo ni pamoja na Idara ya Watu wenye Ulemavu, Baraza la Watu wenye ulemavu,Tume ya UKIMWI, Tume ya Utumishi ya Baraza la Wawakilishi pamoja na Tume ya Kudhibiti Dawa za kulevya.

CDC.jpgCHAI.jpgGlobal Fund Logo.pngLOGO ONE UN.jpgPEPFAR.pngUNAIDS.jpgUNDP.jpgUNFPA.jpgUNICEF.pngUSAID.jpgWHO.pngWORLDBANK_LOGO.jpg