Villagers of South Unguja Pete acquiring knowledge about the fight against AIDS through Jihadhari magazine released by Zanzibar AIDS Commission
Children at ZAPHA+
ZAC Monitoring and Evaluation Coordinator Mr. Ali Kimwaga in one of the M&E meeting
Theatre for Social Development (THESODE) on the stage
Group Picture during World AIDS day climax 2015
Participants attended National Youth Forum in Zanzibar
Group Picture during World AIDS day climax, 1 December 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Watendaji wa Wizara yake ikiwemo Tume ya UKIMWI ambayo imehamishiwa Wizara hiyo.

ZAC Chairperson

Welcome to the Zanzibar AIDS Commission (ZAC) Website. We hope that the ZAC website will serve to give a closer picture about ZAC...Read More

Uzoefu wangu wa kazi ya kujitolea katika Tume ya UKIMWI Zanzibar.

Nilifanya kazi ya kujitolea (volunteer) katika Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC) katika Divisheni ya Uhamasishaji, Utetezi na Mawasiliano kwa takriban mwezi mmoja. Wakati nilipojiunga hapa, nilijifunza mambo mengi.  Sasa nataka kubainisha vitu nilivyojifunza hapa.

Kuanzia tarehe 15 hadi 17 Disemba, kulikuwa na Mafunzo ya stadi za maisha kwa vijana wenye ulemavu-wa kusikia(viziwi)na nilipata fursa ya kujiunga mafunzo na majadiliano kuhusu namna ya kujikinga na UKIMWI na stadi za maisha licha ya vijana kuwa na uelewa kuhusu UKIMWI, lakini hawaelewi vizuri. Wafanya kazi wa ZAC wanawapatia vijana mafunzo kwa kupitia wakalimani kwa kuwatolea  mafunzo hayo kuwashiria kwa vitendo.

Mafunzo mengine pia yalikuwa na faida nyingi. Ninafikiri mafunzo ya stadi za maisha ni muhimu kuliko mafunzo yote kwa vijana. Kwa bahati nzuri mafunzo hayo ya stadi za maisha ni mazuri sana kwa vijana ambao wana ulemavu wa kusikia na kuongea.  

Nilifurahishwa sana kuonana na vijana wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza, licha ya kuwa  nilijitahidi kuwasikiliza kwa makini na niliweza  kufanikiwa kuwafahamu kidogo ingawa ni  muda mfupi tuliofanya mafunzo nao,  lakini tuliweza kupeana mawazo yetu kwa kutumia karatasi na kalamu na kupeana  kumbukumbu za picha katika simu zetu.

Siku nyingine, nilifuatana na wafanyakazi wa ZAC ili kutengeneza makala. Tulitembelea hospitali ya Mnazimmoja, kijiji cha Mkokotoni na Koani pamoja na  afisi ya elimu mjumuisho, na kufanya mahojiano maalum pomoja na daktari na sheha wa shehia ya mkokotoni na koani. Walitaja matatizo ambayo vijiji vyao vinakabiliana navyo siku hadi siku. Pia tulipozungumza na Masheha wa vijiji vya Mkokotoni, Koani  pamoja na Doktari wa Mnazi mmoja, walisema kwamba wanataka  Zanzibar iwe ya amani na pia walisema kuwa Zanzibar bila ya UKIMWI inawezekana.

Hatimaye, ninawashukuru wafanyakazi wa Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC)  kwa kunipokea vizuri na kunipa ushirikiano mzuri na kufanya kazi  vizuri kama nilivyotarajia.

Arisa Haboshi

CDC.jpgCHAI.jpgGlobal Fund Logo.pngLOGO ONE UN.jpgPEPFAR.pngUNAIDS.jpgUNDP.jpgUNFPA.jpgUNICEF.pngUSAID.jpgWHO.pngWORLDBANK_LOGO.jpg