Villagers of South Unguja Pete acquiring knowledge about the fight against AIDS through Jihadhari magazine released by Zanzibar AIDS Commission
Children at ZAPHA+
ZAC Monitoring and Evaluation Coordinator Mr. Ali Kimwaga in one of the M&E meeting
Theatre for Social Development (THESODE) on the stage
Group Picture during World AIDS day climax 2015
Participants attended National Youth Forum in Zanzibar
Group Picture during World AIDS day climax, 1 December 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Watendaji wa Wizara yake ikiwemo Tume ya UKIMWI ambayo imehamishiwa Wizara hiyo.

ZAC Chairperson

Welcome to the Zanzibar AIDS Commission (ZAC) Website. We hope that the ZAC website will serve to give a closer picture about ZAC...Read More

Wanawake wanaoishi katika maeneo ya fukwe za bahari Zanzibar wametakiwa kuvaa nguo zenye heshima ili kuulinda utamaduni wa Mzanzibari na kuondoa vishawishi vinavyopelekea maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na wanakijiji wa Nungwi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati walipotembelewa na waandishi wa jarida hili huko kijijini kwao Nungwi.

Mmoja wa wanakijiji hao aliyejitambulisha kwa jina la Ahmada Haji Pakacha alieleza kwa masikitiko kwamba baadhi ya vijana wa kike kutoka maeneo ya Mkoa huo na nje ya Mkoa huo huonekana katika fukwe huku nguo walizovaa zikiwa fupi na hata zile za ndani zikiwa zinaonekana.

Zanzibar Women

Ameeleza kuwa hali hiyo ni ya kusikitisha sana kwani inaleta taswira potofu kwa jamii Sisi tunachukiwa sana na vitendo vya wanawake kutembea uchi hapa pwani, Mzee Pakacha mwenye umri wa kati ya miaka arobaini na nane alisema.

Mzee Pakacha anaongeza kuwa anavyokumbuka yeye ni kwamba wanawake hata kama wapo kwenye maeneo ya pwani kutafuta riziki lakini hawakuwa wakienda uchi. Mimi nipo hapa kama mvuvi kwa ayami, na vitendo hivi vimejitokeza labda kwa kuiga wazungu wanao tembea na nguo za ndani. Anasema Mzee Pakacha huku akitoa wito kwa jamii kupiga vita mwenendo huo.

Mzee Pakacha anathibitisha kusema kuwa mwanamke hasa Mwafrika anapotembea nusu uchi basi vijana wengi wa kiume huvutika nae na matokeo yake kufanya matendo maovu yanayopelekea maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

Alipoulizwa kwa nini mwafrika avutie zaidi? Amejibu kuwa Mwafrika au mtu mweusi anavutia zaidi anapovaa nguo zinazoonesha maungo yake ya ndani kuliko mzungu kwani anaeleza kuwa mzungu havutii kwa rangi yake.

Ah! Hawa wazungu kutwa anatembea uchi lakini hawana mvuto, mambo hayo afanye mswahili bwana kutaona unavyobadilika, nyavu huiwacha kwanza. Mzee Pakacha anabainisha.

Kwa niaba ya wavuvi wenzake, Mzee Pakacha anatoa wito kwa jamii na Serikali kulivalia njuga tatizo hilo na kuhakikisha kuwa linaondoka mara moja.

Nae msichana mmoja kutoka Mkoa wa Tanga ambae ni mfanyabishara kwenye maeneo hayo anaeleza kuwa heshima ni kitu cha bure kwa hiyo anawaambia vijana wenziwe wa kike na wa kiume kuwa UKIMWI hauchagui kwa hio kila mtu anapaswa kupima afya yake na kujilinda na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

Msichana huyo ambae hakutaka jina lake litajwe anasema kuwa kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni jambo la msingi kwa hiyo wasichana na wavulana wanapaswa kuvaa nguo za heshima.

CDC.jpgCHAI.jpgGlobal Fund Logo.pngLOGO ONE UN.jpgPEPFAR.pngUNAIDS.jpgUNDP.jpgUNFPA.jpgUNICEF.pngUSAID.jpgWHO.pngWORLDBANK_LOGO.jpg