Villagers of South Unguja Pete acquiring knowledge about the fight against AIDS through Jihadhari magazine released by Zanzibar AIDS Commission
Children at ZAPHA+
ZAC Monitoring and Evaluation Coordinator Mr. Ali Kimwaga in one of the M&E meeting
Theatre for Social Development (THESODE) on the stage
Group Picture during World AIDS day climax 2015
Participants attended National Youth Forum in Zanzibar
Group Picture during World AIDS day climax, 1 December 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Watendaji wa Wizara yake ikiwemo Tume ya UKIMWI ambayo imehamishiwa Wizara hiyo.

ZAC Chairperson

Welcome to the Zanzibar AIDS Commission (ZAC) Website. We hope that the ZAC website will serve to give a closer picture about ZAC...Read More

PALE  MNYORORO  UNAPOTOKA ….. !

Juhudi kubwa  zimefanywa  katika kuelimisha  jamii  juu  ya umuhimu wa kutambua  afya zao. Unapomima afya yako majibu ni mawili  tu aidha unaweza kuwa salama bila ya maambukizi ya  virusi  vinavyosababisha UKIMWI au pengine umeambukizwa. Mwamko  uliopo  katika jamii  yetu katika masuala  upimaji ni mkubwa. Kampeni nyingi  zimefanywa  na watu wengi wameitikia  wito. 

Sote  tunatambua  kwamba huduma hii   ya upimaji wa  VVU  ni  ya  hiari. Ingawa katika mazingira  fulani  hasa kwa  mama wajawazito inaweza kuwa ya lazima  kulingana na mahitaji maalum ya  kiafya. Huduma hii imetuwezesha  kuweza kutambua  walau makisio  ya wastani wa  maambukizi ya  VVU  kwa kuangalia kiwango  cha wanaopima  na kiwango cha maambukizi. Taarifa hizi zinatuwezesha hata kupanga  vipaumbele  vya  shughuli kutokana na matokeo ya upimaji   katika  makundi maalum, maeneo na miji, matabaka ya rika la wanajamii  na watu maalum kama mama wajawazito. Kweli hii ni huduma muhimu sana kuwepo katika jamii katika harakati za mapambano dhidi ya UKIMWI. 

Sote  tunakubali  kwamba uwepo wa huduma hii ya ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU ilivyoweza kusaidia  kupunguza  kasi ya maambukizi ya VVU. Kupima afya  yako kuna faida nyingi ;kwanza unatambua afya  yako  aidha kama umeambukizwa ama la;pili unapotambua  afya yako unaweza kuchukua tahadhari za kiafya ya kujilinda usipate maambukizi ama kuwaambukiza  wengine; tatu inakupa fursa ya kuchukua   hatua za tahadhari  katika masuala ya afya  kama vile kujitunza, kufuata matibabu  na mengine. 

Tunafahamu jinsi ya  upimaji kabla ya  ndoa ulivyosaidia kupunguza  kasi ya maambukizi .Upimaji  kwa mama wajawazito umeokoa maisha ya  watoto  wengi kwani huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa  mtoto ipo. Huduma za upimaji za  masafa ( outreach)  zimewafikia  wengi ,jamii  ya watu wa kawaida na makundi maalum. Huduma mjumuisho  iliyoanzishwa katika  vituo  vya umma imesaidia  sana kujua kiwango cha maambukzi.  Pia kwenye shughuli  za kitaifa huduma hizi huwekwa ma watu wengi   hutambua afya zao. Ufanisi  wa ushauri nasaha  na upimaji wa hiari  wa VVU ni  huduma ya lazima katika mapambano  yenye mafanikio juu ya UKIMWI. 

Katika  siku za hivi karibu  huduma  hii imeanza kulega lega.  Malalamiko yanayotolewa na wananchi na wadau wa afya ni makubwa hasa kutokana na upungufu  wa  vifaa vya kupima VVU  yaani HIV  testing  kits .Leo sitazungumzia matatizo ya unyanyapaa yanayoripotiwa katika  vituo vingi.  

Tunatambua kwamba kwa   muongozo  uliopo, Kitengo cha Kinga  Dhidi ya UKIMWI, Malaria Kifua  Kikuu na Ukoma  (ZITLP)  ndio chenye jukumu la  kusimamia utoaji wa  huduma   hii  hasa katika  vituo vya  umma vya  matibabu kwani huduma hii inapaswa kutolewa bure ili iwafikie wananchi waliowengi. Wao ndio wenye jukumu  la   kuratibu huduma hii  ikiwepo kununua ama kupokea kama misaada, kusambaza na kutoa  miongozo ya kitaalamu ni kwa jinsi   inapaswa kutolewa. 

Nilizungumza na Mratibu wa kituo cha huduma rafiki kilichopo Machommane Bi Mmanga Seif alisema kwa baadhi ya miezi   wanakosa  vifaa vya kupimia VVU. Kituo chao cha upimaji kipo Machomanne katika mji  ambao una tabia  na makundi  mengi ya  hatari  yanayoweza kusababisha maambukizi ya VVU (Bi Mmanga picha). 

‘’Tunalazimika  kuwarejesha wateja kwa sababu hatuna. Tunashindwa kufanya kazi  za masafa za upimaji kwa sababu kuna upungufu mkubwa.Tunapoulizia kutoka kitengo husika tunaambiwa hakuna ama zilizopo hazitoshi  kugawa  kwa wanaohitaji’’  Alisema na kuongeza kwamba watu wengi  wanapenda kuja  kituoni hapa kutokana na mazingira  rafiki yaliyopo. 

Hili ni tatizo kubwa linaloikabili huduma hii. Nilizungumza na afisa  mmoja ambae sitataja jina lake anasema ni hatari kwa huduma   hii  muhimu kuwategemea  wafadhili kwa asilimia mia moj 

‘’Hata huyo mfadhili anapokupa  nae  wakati  mwengine  ana masharti yake. Wengine  wanatoa maelekezo kwamba huduma hii isitolewe kwe kazi  za masafa ( outreach ), wengine anasema itolewe  kuyafika makundi maalum  tu “  Alisema  na kubainisha kwamba  wanashindwa  kutoa huduma hii hata jamii ya kawaida  ( general population).

Pia nilizungumza na wanaofanya kazi za  masafa hapa Pemba kuyafikia makundi  maalum walisema ni shida  pia. Wakati mwengine wanashindwa kupima watu  afya zao kwa   sababu  wamekosa vifaa. Wanalazimika kutoa ushauri tu na huduma  nyengine. Hii ni hatari hasa kwa vile kujua afya  kwa makundi haya   maalum ni muhimu sana   katika mapambano dhidi ya  UKIMWI.

‘’Unapokwenda kutoa elimu ya ushauri  na huduma  nyengine  na watu  wakawa na hamu ya kuangalia afya  zao na ukawajibu huna vifaa vya upimaji hawakuelewi umekwenda kufanya nini! ‘’ Kilisema chanzo chetu cha habari. 

Yapo matatizo makubwa  ya upatikanaji wa huduma  hii. Taratibu  za uagiziaji pia  ( procurement) na usambazaji  si za kuridhisha.

Nilitembelea baadhi ya  hospitali  za binafsi  ambazo pia zinatoa huduma hii  tatizo ni hilo hilo 

‘’Sisi hapa tumefunga huduma hii  .Wateja wanasumbuka lakini hatuna  vya kufanya .Tunapokua na haja ya huduma hii  huwalazimisha wateja waende  kwengine .Huko wakikosa kwa kweli inakua shida ‘’  Alisema

Nini tufanye ili kuhakikisha kwamba  huduma hii ya ushauri nasaha  na upimaji wa hiari  wa VVU inatolewa katika   vituo vya umma  na  binafsi  bila   ya usumbufu wowote ni  jambo la msingi sana kwani ni huduma muhimu na  ya  lazim. La  msingi  ni kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma hii iliyopo na   kuondoa urasimu.Tunatambua kwamba huduma hii ni ya gharama kubwa  lakini  kwa kutegemea ufadhili  kwa  asilimia kubwa ni jambo la mashaka. Tukiangalia wastani  wa kiwango cha upimaji  kwa mwaka hapa Zanzibar  na idadi ya watu  wetu  tunaweza kumudu gharama hizi na kuondosha usumbufu 

Nakumbusha  tu , mapambano  dhidi ya UKIMWI ni kama mnyororo  wa baskeli kwani kijino kimoja tu kinapotoka kwenye ringi lake  safari huishia hapo. Natambua umuhimu  wa ufanisi wa huduma hii.Tunajua ni jinsi gani imesaidia katika mapambano dhidi ya UKIMWI . Inawezekana  kulifanikisha  hili ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake. 

 

CDC.jpgCHAI.jpgGlobal Fund Logo.pngLOGO ONE UN.jpgPEPFAR.pngUNAIDS.jpgUNDP.jpgUNFPA.jpgUNICEF.pngUSAID.jpgWHO.pngWORLDBANK_LOGO.jpg